Wednesday, 3 May 2017

MABIBI HARUSI WAPEWA SILAA ZA KUJILINDA



Mamia ya mabibi harusi katika arusi ya halaiki wamepewa silaha ya kujilinda dhidi ya waume zao wanaponyanyaswa.
Mamia ya mabibi harusi Nchini INDIA, katika arusi ya halaiki wamepewa silaha ya kujilinda dhidi ya waume zao wanaponyanyaswa.
Ujumbe kama ''tumia dhidi ya mlevi'' umeandikwa katika ubao huo ulio na urefu wa sentimita 40 na hutumika sana kundoa uchafu katika nguo.
Gopal Bhargava , waziri wa maswala ya ndani nchini humo alisema kuwa anataka kuangazia swala la unyanyasaji wa wanawake waliopo katika ndoa.
Aliwaambia kujaribu kuafikiana na wanaume zao kabla ya kutumia ubao huo unaojulikana kama Mogri na hutumika sana kuondoa uchafu katika nguo,'' fanyeni mazungumzo mwanzo'',alisema.
Bwana Bhargava alichapisha picha za mabibi harusi waliobeba mbao hizo katika ukurasa wake wa facebook.
Aliambia chombo cha habari cha AFP kwamba amekuwa na wasiwasi kuhusu idadi ya wanawake wa mashambani ambao hunyanyaswa na wanaume walevi
''Wanawake wanasema kwamba kila wanaume wao wanapokunywa na kulewa chakari wanawapiga''.
''Fedha walizohifadhi huchukuliwa na kutumiwa kununua pombe'', alisema.
''Hakuna dhamira ya kuwachochea wanawake kufanya ghasia lakini ubao huu ni wa kujilinda dhidi ya ghasia''.Mabibi harusi hupewa ubao ili kujilinda dhidi ya unyanyasaji unaofanywa na wanaume zao
Bwana Bhargava anayetoka katika chama cha Janata Party cha waziri mkuu wa India Narendra Mody anasema kuwa ameagiza mbao 10,000 kwa jumla.
Takriban mabibi harusi 700 walipokea mbao hizo katika harusi ya halaiki nyumbani kwake huko Garhakota wikendi iliopita.
Harusi za halaki hufanywa ili kuwasaidia watu wenye mapato ya chini kufunga ndoa bila kulipia hafla hiyo.
Vyombo vya habari vinasema kuwa ilikuwa njia ya kupata uungwaji mkono kabla ya uchaguzi wa mwaka ujao.Mabibi harusi hupewa ubao ili kujilinda dhidi ya unyanyasaji unaofanywa na wanaume zao

No comments:

Post a Comment