Habari ya asubuhi, usikokose kupita huku kila siku ili uweze kusoma Habari kubwa kwenye magazeti yako pendwa.Karibu
Pata habari za kisiasa,michezo,biashara na vichekesho mbalili.Pia hamasika kupitia makala mbalili Usisahau udaku,ubuyu,umbea wa town pia utapata
Sunday, 7 May 2017
Saturday, 6 May 2017
HIZI NDIZO FAIDA ZA MAJANI YA MAPARACHICHI
Zifuatazo ni faida ya majani ya mparachichi.
Majani ya parachichi humsaidia mwanamke ambaye hupata maumivu wakati wa hedhi.
Unachotakiwa kufanya ni;
Chukua majani kiasi ya mparachichi, kisha yachemshe kwenye maji lita
moja, ukijiridhisha yamekwisha chemka epua kisha yaache yapoe, kisha
anza kunywa maji hayo kiasi cha nusu kikombe cha chai, kunywa muda wa
asubuhi na jioni kwa muda wa wiki moja utaona mabadiliko.
1. Majani ya mparachichi husaidia sana kuongeza kiwango cha maziwa kwa kinamama.
2. Unachotakiwa kufanya ni
Tatatafuna jani moja la parachichi kila siku, lakini hakikisha jani unalotafuna liwe katika hali ya safi na umeliosha vizuri.
Tatatafuna jani moja la parachichi kila siku, lakini hakikisha jani unalotafuna liwe katika hali ya safi na umeliosha vizuri.
3. Pia majani haya ya mparachichi ni msaada sana katika kutibu majeraha,
ili kufanikiwa katika hili unapaswa kusaga majani hayo kisha weka
kwenye sehemu yenye jeraha na utaona mafanikio,
4.Majani ya mparachichi pia husaidia kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Pia tunda la parachichi linafaida nyingi sana kwana ni tamu ukila kama lenyewe lakini pia ni tiba ya magonjwa mbalili , juice yake pia ni tiba.
Hizo ni faida chache kati ya nyingi ambazo hutibika na majani ya parachichi.
Wednesday, 3 May 2017
MABIBI HARUSI WAPEWA SILAA ZA KUJILINDA
Mamia ya mabibi harusi Nchini INDIA, katika arusi ya halaiki wamepewa silaha ya kujilinda dhidi ya waume zao wanaponyanyaswa.
Ujumbe
kama ''tumia dhidi ya mlevi'' umeandikwa katika ubao huo ulio na urefu
wa sentimita 40 na hutumika sana kundoa uchafu katika nguo.Gopal Bhargava , waziri wa maswala ya ndani nchini humo alisema kuwa anataka kuangazia swala la unyanyasaji wa wanawake waliopo katika ndoa.
Aliwaambia kujaribu kuafikiana na wanaume zao kabla ya kutumia ubao huo unaojulikana kama Mogri na hutumika sana kuondoa uchafu katika nguo,'' fanyeni mazungumzo mwanzo'',alisema.
Bwana Bhargava alichapisha picha za mabibi harusi waliobeba mbao hizo katika ukurasa wake wa facebook.
Aliambia chombo cha habari cha AFP kwamba amekuwa na wasiwasi kuhusu idadi ya wanawake wa mashambani ambao hunyanyaswa na wanaume walevi
''Wanawake wanasema kwamba kila wanaume wao wanapokunywa na kulewa chakari wanawapiga''.
''Fedha walizohifadhi huchukuliwa na kutumiwa kununua pombe'', alisema.
''Hakuna dhamira ya kuwachochea wanawake kufanya ghasia lakini ubao huu ni wa kujilinda dhidi ya ghasia''.
Bwana Bhargava anayetoka katika chama cha Janata Party cha waziri mkuu wa India Narendra Mody anasema kuwa ameagiza mbao 10,000 kwa jumla.
Takriban mabibi harusi 700 walipokea mbao hizo katika harusi ya halaiki nyumbani kwake huko Garhakota wikendi iliopita.
Harusi za halaki hufanywa ili kuwasaidia watu wenye mapato ya chini kufunga ndoa bila kulipia hafla hiyo.
Vyombo vya habari vinasema kuwa ilikuwa njia ya kupata uungwaji mkono kabla ya uchaguzi wa mwaka ujao.
Monday, 1 May 2017
Subscribe to:
Posts (Atom)